Magazetini Jumanne Julai 20, 2021: Jubilee kuelekea kortini kupinga ushindi wa UDA


Na Collins Oluyali

Magazeti ya yanaripoti kuhusu ziara ya kiongozi wa Orange Democratic Movement (ODM) Raila Odinga na hasimu wake kisiasa naibu rais William Ruto eneo la Pwani katika harakati zao za kutafuta kura.

Magazeti haya pia yanagusia mvutano wa kisiasa kati ya Ruto na Uhuru eneo la Mt Kenya uchaguzi mkuu wa 2022 unapokaribia.

image

Daily Nation

Gazeti hili limeangazia mkutano wa leo Jumanne, Julai 20, wa viongozi wa muungano wa One Kenya Alliance (OKA) wa kupokea mapendekezo ya kumteua mgombea wa urais.

Viongozi wa OKA– Seneta wa Baringo Gideon Moi mwenzake wa Bungoma Moses Wetang’ula, Kalonzo Musyoka (Wiper Kenya), na Musalia Mudavadi (Amani National Congress), wako njia panda kuhusu atakayekabiliana na Ruto mwaka 2022.

Daily Nation pia linaripoti kuwa baba yake marehemu afisa wa polisi Caroline Kangogo amepuzilia mbali madai kuwa binti yake aliuawa.

image

The Standard

Huku maelfu ya Waislamu nchini wakisherehekea Eid Ul-Adha, The Standard linataja sababu za waumini hao kuchinja wanyama sikukuu hiyo baada ya Eid-Ul-Fitr, ambayo huandaliwa kufuatia Ramadhan.

Baada ya maombi ya Eid, Waislamu huchinja wanyama kukumbuka namna Ibrahimu alikuwa tayari kumtoa mwanawe kama kafara.

Gazeti hili pia limeguzia mauaji ya mwanamazingira mwenye umri wa miaka 64, Joannah Stutchbury aliyeuawa katika kaunti ya Kiambu Alhamisi, Julai 15.

Matokeo ya upasuaji yaliyotolewa na mwanapatholojia mkuu wa serikali Johansen Oduor yalibaini kuwa Joanna alipigwa risasi mara sita.

image

Taifa Leo

Kulingana na chapisho hili, mgombeaji wa chama cha Jubilee katika uchaguzi mdogo wa Kiambaa, Kariri Njama, amekataa kushindwa baada ya ushindi telezi wa mwaniaji wa United Democratic Alliance (UDA), John Wanjiku.

Chama hicho tawala sasa kimeapa kuwasilisha kesi kortini kupinga matokeo hayo.

Jubilee kimelaumu Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa kushindwa huko wakitaka kura hizo zihesabiwe upya.

Gazeti hili pia limeripotia uvamizi wa Raila na Ruto eneo la Pwani. Mpango wa Raila ni kuzuia kumalizwa kisiasa na Ruto, ambaye pia yuko makini kuzima umaarufu wa chama cha ODM, ambacho kimekuwa kikizoa kura nyingi eneo hilo tangu 2007.

image

The Star

Kulingana na gazeti hili, serikali inapanga kuzuia vyuo vikuu kuwachukua wanafunzi wa diploma na vyeti katika mabadiliko yanayofanyiwa kozi.

Waziri wa Elimu George Magoha anapendekeza vyuo vikuu vizingatie masomo ya digrii pekee na utafiti. Wizara hiyo, katika mapendekezo yake, inataka kozi za diploma na cheti kuondolewa.

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.