Category Archives: TL Sportsline

Sports Roundup: Matukio muhimu viwanjani wikendi


Na Tom Lutali

Wikendi hii imeshuhudiwa matukio mbalimbali kutoka riadha hadi kandanda.

Wakenya wang’aa katika riadha

Kwenye mashindano yanayoendelea ya Africa Duathtop Championship nchini Namibia upande wa akina dada, Mkenya Yvonne Zilpa alishinda nishani ya dhahabu .

Upande wa wanaume, Elisha Rotich alimaliza wa kwanza Kwa muda wa dakika 2:04:18 na kuandikisha muda bora wake wa binafsi. Kariuki Mungai alimaliza wa tatu.

Wanariadha wa Kenya waling’aa wikendi hii. (Picha- hisani)

United yapata kichapo huku Liverpool na Chelsea ziking’aa

Miamba wa Anfield Liverpool waliwaadhibu Watford 5-0 na kuendeleza rekodi yake ya kutoshindwa msimu huu.

Kwingineko, masaibu ya mashetani wakendu Manchester Unitedyaliendelea Jumamosi ugani Kingpower baada ya kufungwa 4-2 na Leicester City.

Mohamed Salah akiwaongoza wenzake kusherehekea ushindi wa Liverpool. (Picha- hisani)

Kichapo hicho kimezidisha shinikizo la kutimuliwa kwa mkufunzi Ole Gunner.

Kwingineko Manchester City waliwashinda Burnely 2-0 huku vijana wake Thomas Tuchel Chelsea wakiendeleza matokeo mazuri kwa kuwafunga limbukeni Brentford 1-0 na kuzidi kileleni mwa ligi kuu.

Totenham Hotspurs waliwapigisha magoti Newcastle 3-2 ugani St James Park mbele ya wamiliki wapya.

Ratiba ya UCL: Mabingwa watetezi Chelsea kukabili Juventus


Na Tom Lutali

Chelsea watakuwa wageni wa Juventus usiku wa leo katika kipute cha kuwania kombe la klabu bingwa Uropa (UCL).

Mabingwa hao watetezi wanapania kujikwamua baada ya kufungwa Jumamosi na Manchester City 1-0 kwo Stamford Bridge katika ngaramba ya EPL.
Juventus, kwa upande wao, wanataka kuendeleza msusuru wa matokeo mazuri maana watakuwa wanatafuta ushindi wao wa tano katika michuano yao yote msimu huu.
Chelsea watakuwa bila kiungo wao muhimu raia wa Ufaranza NG’olo Kante ambaye anaugua.
Juventus nao hawatakuwa na mashambuliaji wao matata Alvaro Morota na Paulo Dybala ambao wanauguza majeraha.

Ratiba ya leo katika UCL
• Atalanta vs Young Boys– 19:45
• Zenit vs Malmo– 19:45
• Bayern Munich vs Dynamo Kyiv– 22:00
• RB Salzburg vs Lille– 22:00
• Juventus vs Chelsea– 22:00
• Manchester United vs Villarreal– 22:00

Sports Roundup: Arsenal yang’aa huku Chelsea ikifedheheshwa na City


Ligi kuu ya Uingereza inaingia wiki ya sita huku kukishuhudiwa matukio ya kufana katika mechi mbalimbali wikendi iliyopita kama anavyosimulia Tom Lutali.

Kichapo cha Chelsea

Manchester City waliiwafunga Chelsea 1-0 ugani Stamford Bridge. Vijana wake Pep Guadiola walionyesha nia tangu sekunde ya kwanza wakionekana kuwalemea vijana wake Thomas Tuchel ambao walionekana dhaifu hasa katika safu ya kati.

Bao la pekee la City lilifungwa na Gabriel Jesus kipindi cha pili.

Gabriel Jesus akitia kimyani bao la City dhidi ya Chelsea Jumamosi. (Picha kwa hisani ya Mirror)

Villa yaifadhaisha United

Wakati huo huo, Aston Villa waliwaduwaza Manchester City 1-0 ugani Old Trafford. Masheteni hao wekundu walipoteza mkwaju wa penalti dakika za mwisho ambapo Bruno Fernandes alipayusha juu goli.

Hi ni mechi ya pili vijana hao wa Ole Gunner wanapoteza mtawalia.

United ilipokea kichapo kutoka kwa Aston Villa Jumamosi. Picha- hisani

Brentford yawashika Liverpool mateka


Katika mechi ya kusisimua, limbukeni Brentford walitoka sare dhidi ya miamba Liverpool ya 3-3.

Mshambulizi wa timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah alifunga bao lake la mia moja katika mechi hiyo. Baada ya sare hiyo ya kuudhi kwa The Reds, Liverpool walichupa kileleni kwa alama 14 alama moja zaidi ya Manchester City na Chelsea mtawalia.

Brentford waliwashika mateka Liverpool Jumamosi na kutoka sare. (Picha kwa hisani ya Independent)


Debi ya London Kaskazini

Arsenali waliwaadhibu Tottenham 3-1 ugani Emirates Stadium. Mabingwa hao wa 2004 walifunga mabao yao matatu kipindi cha kwanza na kuwadhalilisha Tottenham ambao walionekana wanyonge. Mabao ya Arsenali yalifungwa na Smith Rowe dakika ya ’12, Nahodha Abumeyang dakika ya ’26 na Bukayo Saka dakika ’34.

Bao la pekee la Tottenham Hotspurs lilifungwa na Son dakika ya ’78.

Kwa sasa vijana wa Michael Arteta wamepanda hadi nambari ya 10 na alama 9.

Arsenal walinga’aa jana dhidi ya Tottenham. (Picha kwa hisani ya 90min)

Sports Roundup: Matukio muhimu ya spoti wikendi


Wikendi hii imeshuhudia matukio mseto viwanjani kama inavyosimuliwa na Tom Lutali na FK Zack

Omanyala aweka rekodi mpya ya mbio za 100m

Ferdinand Omanyala amekuwa Mkenya wa hivi punde kuweka rekodi mpya katika mbio za mita 100.

Kwenye mbio za Keino Classic Jumamosi, Omanyala alimaliza wa pili kwa muda wa sekunde 9.76 nyuma ya Mmarekani Trayvok aliyemaliza wa kwanza.

Pigo la Malkia Strikers

Kwingineko, timu ya taifa ya akina dada Malkia Strikers ilipoteza fainali yao dhidi ya vipusa kutoka Cameroon kwenye ubingwa wa Afrika .

Cameroon sasa watawakilisha Afrika kwenye mashindano yajayo ya Ulimwengu.

Ubingwa wa Police FC

Klabu ya Police FC imepandishwa daraja baada ya kuifunga Vihiga United Jumapili kwa jumla ya mabao 2–0.

Kwa sasa Police FC watashiriki ligi kuu ya FKFPL msimu ujao.

image
Police FC imepandishwa daraja baada ya kuicharaza Vihiga United. Picha – hisani

Matukio katika Premier League

Ughaibuni, klabu ya Liverpool iliwaadhibu Crystal Palace 3-0 huku mchezaji Muhammad Salah akiifunga The Reds mabao mawili na  Sadio Mane moja.

Sala sasa amefikisha mabao 100 katika ligi kuu ya Uingereza.

Manchester City waliambulia sare ya 0-0 dhidi ya Southampton huku vijana wake Ole Gunner Manchester United wakipata ushindi wa 2-1 dhidi Westham.

Kwenye London Derby ugani kwa Tottenham Hotspurs,  Chelsea walikosa adabu za mgeni Kwa kuwafunga wenyeji 3–0.

Mabao ya Chelsea yalifungwa na Thiago Silva, Kante na Antonio Rudiger.

Ubingwa wa Tusker

Washindi wa ligi kuu nchini Tusker waliilaza Arta Solar 7 kutoka Djibouti 3-0 katika mechi yao ya marudiano katika uga wa Nyayo.

Shami Kibwana, Ibrahim Joshua na Deogratius Ojok walikua wafungaji kwa upande wa Tusker.

Mkondo wa kwanza  kule Djibouti uliisha kwa timu zote kutoka sare ya 1-1 na baada ya ushindi huu Tusker inamaliza kwa jumla ya mabao 4-1. Ushindi huu umeiwezesha Tusker kusonga kwa hatua ya kwanza ya Caf Champions League watakapokutana na Zamalek.