Malala atishia kujiondoa OKA iwapo itashirikiana na Raila


Seneta wa Kakamega Cleophas Malala ametishia kujiondoa kwenye muungano wa One Kenya Alliance (OKA) iwapo utashirikiana na kiongozi wa Orange Democratic Movement (ODM) Raila Odinga.

Akizungumza mjini Bungoma,Ijumaa wakati wa ziara ya OKA kwa wapiga kura, Malala alimshutumu Raila kwa kuwapumbaza viongozi wa jamii ya Waluhya na kuzungumza nao kwa utamu tu kipindi cha uchaguzi kinapokaribia.

Alimtaka kiongozi huyo wa ODM kujitenga na masuala ya OKA na kuangazia azma yake ya urais.

“Nataka Raila apate hili waziwazi. Tafadhali epuka kutema mate kwa ajili ya muungano wa OKA. Endelea tu kufanya kampeni zako kama sisi tunavyofanya zetu. Timu hii ndiyo itakayounda serikali ijayo,” Malala alisema.

Malala, ambaye ana azma ya kuwa gavana wa Kakamega, aliongezea kuwa wakati wa mapatano kati ya Raila na rais Uhuru Kenyatta, Raila alienda pekee yake bila kuwakumbuka vinara wenzake wa NASA ambao walitembea pamoja wakati wa uchaguzi wa 2017.

“Nataka Wetangula, Mudavadi na Kalonzo wapate somo kutoka kwa Raila. Baada ya kuafikiana na rais Kenyatta, alisahau masuala ya NASA,” akasema.

Aliwataka wakuu wa OKA kuzingatia na kutoa rais ajaye wa Jamhuri ya Kenya.

Hata hivyo, Malala alimlaumu kiongozi wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka kwa kumwalika Raila Odinga katika uzinduzi wa azma yake ya urais, akisema kuwa Raila ni wakati uliopita na hafai kuhusika katika kupanga OKA.

Akijibu, Kalonzo alimwambia Malala kwamba OKA haiwezi kumfukuza yeyote ambaye yuko tayari kuwaunga mkono, badala yake muungano huo utakaribisha viongozi kutoka makabila yote ya Kenya ili kuhakikisha kwamba wanamtoa rais ajaye.

Savula promises to set up cancer fund if elected Kakamega governor


Outspoken Lugari Member of Parliament, Ayub Savula, has promised that – if elected governor of Kakamega County in next year’s general elections – he will put up a cancer fund that will offer free treatment of the disease.

During a function in his constituency a few days ago, the two-term legislator, who is under fire for his controversial track record for the nearly 10 years he has been in charge of Lugari, also promised to establish a cancer center in Kakamega town.

His administration will also have in place a program that will see a 100-bed capacity health facility put up in every ward, he said.

Divisive politics

The ANC party leader also called upon politicians to stop divisive politics from use of inciteful language.

Savula, who is eager to succeed Wycliffe Oparanya, expressed concern that the inflammatory words heard from leaders across the country is a threat to national peace as the 2022 general elections fast approach.

He is afraid that what was witnessed after the 2007/2008 general elections might repeat, he suggested.

The legislature claimed that the only leader fit for the country as at now is his ANC boss, Musalia Mudavadi, who, through his Uchumi Bora slogan, has announced interest to lead the country.

Magazetini Jumatatu: Hakuna huduma za serikali bila chanjo ya Covid-19


Magazeti ya Jumatatu, Novemba 22, yameripotia pakubwa siasa za 2022 huku kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka akiitisha mkutano wa kujadili nafasi yake ya kuwania urais.

Magazeti haya pia yamegusia masharti mapya ya Wizara ya Afya ya kuwafungia nje wale ambao hawajachanjwa dhidi ya COVID-19 kupata huduma za serikali.

The Star

Katika The Star, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka anatazamiwa kufanya mkutano na wajumbe wa chama hicho kuhusu azma yake ya kugombea urais 2022.

Makamu huyo wa zamani wa rais amekuwa njia panda iwapo atawania kiti hicho na, wakati mmoja, kudokeza kuwa anataka kuungana na naibu rais William Ruto.

Mkutano wa wajumbe wa chama hicho utatoa mwelekeo kuhusu hatma yake kisiasa. Mwaka ujao, Kalonzo atakuwa anajaribu mara ya pili kuwania urais iwapo atagombea. Katika chaguzi mbili zilizopita amekuwa mgombea mwenza wa Raila.

The Standard

Muungano wa One Kenya Alliance (OKA) umeshikilia kuwa utaendelea na mpango wake wa kumteua mgombeaji wao wa urais mwakani.

Muungano huo unawaleta pamoja Kalonzo wa Wiper, kinara wa KANU Gideon Moi, Musalia Mudavadi wa ANC na mwenzake wa Ford Kenya Moses Wetangula.
Mnamo Jumapili, Novemba 21, wanne hao walifanya mikutano kadhaa ya hadhara mjini Naivasha ambapo walipigia debe muungano wao licha ya mvutano baina yao.

Kalonzo alifutilia mbali ripoti za vyombo vya habari kuwa OKA unakaribia kuvunjika, akifichua kwamba wanatumainia kuwaalika wanachama wengine.

Kumekuwa na ripoti ya malumbano OKA huku vyama tanzu vikilaumiana kwa usaliti. Cleophas Malala alikuwa amekashifu KANU kwa kulemaza muungano huo.

Daily Nation

Gazeti hili linaripoti vita kati ya aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga na wakili Ahmednassir Abdullahi almaarufu Grand Mullah.

Maraga amefungua kesi dhidi ya Grand Mullah kuhusiana na madai ya kumharibia jina. Wakili huyo alidai kuwa Maraga alipata cheo cha Jaji Mkuu kupitia kushawishi idara ya mahakama kila mara.

Kulingana na Grand Mullah, Maraga aliwahi kupokea hongo ya Ksh 200 milioni kutoka kwa mmoja wa majaji wa Mahakama ya Upeo.

People Daily

People Daily inaripoti kuwa Wakenya ambao hawajachanjwa hawatapokea huduma za serikali kuanzia Disemba 21, 2021.

Kulingana na Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, yeyote anayetafuta huduma ya serikali ni lazima awe na cheti cha kupokea chanjo ya COVID-19.

Kagwe alisema kuwa wizara yake, ikishirikiana na serikali za kaunti na washikadau wengine, itafanya zoezi ya kuchanja halaiki kwa siku kumi kuanzia Novemba 26.

“Hakuna aliyesema chanjo ni lazima, lakini ukitaka huduma za serikali lazima uchanjwe dhidi ya virusi hivyo,” alisema Kagwe.

Huduma hizo za serikali ni kama vile KRA, elimu, uhamiaji, afya, NTSA, na bandari.

Taifa Leo

Gazeti hili limeripoti kupungua kwa makali ya Ruto kuelekea uchaguzi mkuu wa 2022. Utafiti uliofanywa na Tifa ulionyesha kuwa umaarufu wa naib rais unaendelea kudidimia licha ya kuongoza katika mbio za kuwania urais.

Kura ya maoni ilionyesha kuwa Ruto ana umaarufu wa 38% akifuatwa na Raila, ambaye ana 23%.

Hata hivyo, utafiti huo ulibaini kwamba umaarufu wa Ruto unapungua huku wa Raila ukiendelea kuimarika.

Katika eneo la Mlima Kenya, Raila ana uungwaji mkono mkubwa, akiungwa mkono na magavana wote kando na Gavana wa Kirinyaga, Anne Waiguru, ambaye alihama Jubilee na kujiunga na UDA.

Mautuma: Msichana mlemavu, 21, apokezwa kiti cha magurudumu na mhisani


Familia moja kutoka kijiji cha Mbagara, wadi ya Mautuma, Lugari, imejawa na furaha tele baada ya mwanao mlemavu kupata kiti cha magurudumu kutoka kwa mhisani.

Nick Luvai, mhisani huyo, anasema aliguswa sana na swala la Shafuu Shikobe, msichana wa umri wa miaka 21 ambaye ana ulemavu wa miguu, ndipo akashiriana na Tom Lutali, ambaye ni mwandishi wa Lugari Daily, kununua na kumkabidhi kiti hicho.

Kando na kiti cha magurudumu, Luvai alimfadhili Shafuu na sukari na nguo.

Mamake Shafuu, Zamzam Mwanzanze, ameonyesha kuridhishwa na kitendo hicho cha usamaria wema huku akidhibitisha kuwa wamekuwa wakipitia wakati mgumu sana kulea mwanao ambaye alizaliwa na hali hiyo.

“Tangu nihamie huku, sijawahi kuona mtu akinisaidia jinsi naweza lea mtoto huyu. Nimeshukuru sana na Mungu awabariki,” alisema Bi Zamzam, ambaye ni mjane na anaishi katika ulitima.

Anaongezea kuwa amekuwa akisumbuliwa na mwanawe anayetaka kupelekwa shuleni akasome lakini hana uwezo wa kumlipia karo.

“Kwa sasa nimepata nafuu kiasi maana sitakuwa nambeba tu ila atakuwa akisukumwa akiwa amekalia kiti hiki cha magurudumu,” alisema Bi Zamzam kwa tabasamu.