Category Archives: World News

Major world news.

Hakainde Hichilema ashinda uchaguzi Zambia baada ya kujaribu mara sita


Hakainde Hichilema hatimaye ametangazwa mshindi katika kinyang’anyiro cha urais Zambia akimbwaga Edgar Lungu anayeshikilia madaraka sasa.

Hichilema amepata ushindi baada ya kujaribu hii ikiwa ni mara ya sita

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo imemtangaza Hakainde Hichilema kuwa mshindi katika uchaguzi uliofanyika Alhamisi iliyopita, akimbwaga rais wa sasa Edgar Lungu.

Hakainde Hichilema amembwaga rais wa sasa wa Zambia Edgar Lungu katika uchaguzi. Picha– hisani

Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi ya Zambia Esau Chulu ameyatangaza matokeo rasmi asubuhi ya leo Jumatatu, baada ya kupatikana hesabu za majimbo yote lisipokuwa moja tu.

Hesabu hizo zimeonyesha kuwa Hakainde Hichilema wa chama cha United Party for National Development (UPND) amepata kura 2,810,777; akimpita kwa mbali rais wa sasa Edgar Lungu kutoka chama cha Patriotic Front (PF) aliyepata kura 1,814,201.

Wapiga kura milioni saba walikuwa wamejiandikisha kupiga kura katika nchi hiyo yenye idadi jumla ya raia milioni 19.

Hapo jana rais Lungu alisema uchaguzi huo haukuendeshwa katika mazingira huru na haki, na kutishia kukataa matokeo yake.

India: Raia watafuta njia mbadala hospitali zikilemewa na Covid-19


Na Tom Lutali

Huku hospitali jiji kuu la Delhi na miji mingine mikuu zikikosa vitanda vya kulaza wagonjwa, wananchi wamelazimika kutafuta njia mbadala ya kujitibu wakiwa nyumbani. Wengi wameingilia biashara ya magendo ambapo baadhi ya vifaa muhimu kama  dawa na oxyjeni vinauzwa.

Jumatatu, India imerekodi visa 352,991 chini ya saa 24, ambavyo ndivyo vingi zaidi duniani kwa muda huo.

Anshu Priya, raia wa India, hakuweza kupata kitanda Delhi na mji wa Noida ili amlaze baba mkwe wake. Hali ya babake ya kiafya inazidi kudorora akiwa ametafuta oxyjeni Jumapili kutwa bila mafanikio.

image
Hospitali India zimelemewa na Covid-19. Picha | Hisani

Watu wengi hawana uwezo wa kumudu kununua bidhaa hizo kwa sasa ambayo bei yake imepanda maradufu. Kuna ripoti kwamba wagonjwa wengi wanaaga dunia milangoni pa hospitali kwa kukosa kumudu kununua bidhaa hizo muhimu kama dawa na oxyjeni.

Ila kwa wale ambao wana uwezo wa kununua bidhaa hizo, wanakodi daktari kuja kutibu mgonjwa wao nyumbani.

___________
To place your advertisement, contact 0721747146

Uingereza yasitisha safari ya kuingia nchini humo kwa raia wa India


Na Tom Lutali

India imeongezwa kwa orodha ya nchi ambazo zimepigwa marufuku ya raia wake kusafiri kuingia Uingereza kutokana na aina mpya ya Covid Vibrant, katibu mkuu wa wizara ya afya amesema.

Kuanzia April 23, wananchi wa India ambao watakuwa wamesafiri Uingereza hawataruhusiwa kuingia. Wale ambao wana pasipoti wataruhusiwa ila watakaa karantini kwa siku kumi wakisubiri usahisishaji wa serikali.

Matt Honcock amesema kumekuwa na visa 103 Uingereza vya Vibrant Covid kutoka India.
Kwa mjibu wa taarifa kutoka House of Commons Jumatatu, katibu huyo amesema nyingi ya visa vya vVbrant Covid B 1.617 vimesambaa hadi kwa usafiri wa kimataifa.

image
Ndege ya Uingereza. Picha | Hisani

Alisema sampuli zimechukuliwa ili kubaini ikiwa Vibrant Covid ina tabia sawia ama inakataa chanjo.

Wale wanaingia Uingereza ni lazima wawe na vyeti vyao vya kudhibitisha kwamba hawana virusi hivyo na ni chini ya saa 72 kabla ya kuruhusiwa kuingia.

Hayo yanajiri huku serikali ya Kenya ikizidi kukaza kamba katika kaunti tano zilizofungwa. Polisi wameonekana wakishika doria usiku kucha ili kuhakikisha masharti yaliyowekwa yanafuatwa. Mfano Nairobi, wananchi waliopatikana wakiwa nje saa za kafyu walikesha usiku kucha na maafisa wa polisi.

___________
Do you have any comments or suggestions on our stories? Kindly reach out to us on phone: 0721747146 or email: lugaridaily@gmail.com. Thank you for following, we value you so much.

No coalition talks, say Murkomen and Mbadi


By Moses Kibwana

Elgeyo Marakwet Senator Kipchumba Murkomen and ODM chairman John Mbadi have now come out strongly and reassured their supporters that neither Raila Odinga nor William Ruto are having plans to jointly form an alliance which will lead the two of them to the hotly contested 2022 presidential elections.

Speaking in an interview in a leading television station yesternight, Mbadi said the ODM party is focused on BBI and that it had not joined any form of talks with anyone about a coalition.

image
ODM leader Raila Odinga (left) and DP William Ruto.

In his response, Murkomen added that although the ‘Hustler Nation’ believed in Raila Odinga as the only credible competitor they have come 2022, they have never been in any coalition talks with ODM. When asked if an alliance between the two leaders could work, Murkomen adamantly refused, comparing the two leaders and their parties with the US Republican and Democratic parties, which can never work together.

This comes a few weeks after Ruto’s interview with a radio station in which he expressed readiness to work with all like-minded politicians who have the same dreams for Kenya as he does.

Kenyans now await to see the coming up of new alliances as 2022 elections draw nearby. Already formed is the One Kenya Alliance by Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi, Moses Wetangula and Gideon Moi.