Category Archives: Sports News

A comprehensive sports coverage.

Sports Roundup: Matukio muhimu viwanjani wikendi


Na Tom Lutali

Wikendi hii imeshuhudiwa matukio mbalimbali kutoka riadha hadi kandanda.

Wakenya wang’aa katika riadha

Kwenye mashindano yanayoendelea ya Africa Duathtop Championship nchini Namibia upande wa akina dada, Mkenya Yvonne Zilpa alishinda nishani ya dhahabu .

Upande wa wanaume, Elisha Rotich alimaliza wa kwanza Kwa muda wa dakika 2:04:18 na kuandikisha muda bora wake wa binafsi. Kariuki Mungai alimaliza wa tatu.

Wanariadha wa Kenya waling’aa wikendi hii. (Picha- hisani)

United yapata kichapo huku Liverpool na Chelsea ziking’aa

Miamba wa Anfield Liverpool waliwaadhibu Watford 5-0 na kuendeleza rekodi yake ya kutoshindwa msimu huu.

Kwingineko, masaibu ya mashetani wakendu Manchester Unitedyaliendelea Jumamosi ugani Kingpower baada ya kufungwa 4-2 na Leicester City.

Mohamed Salah akiwaongoza wenzake kusherehekea ushindi wa Liverpool. (Picha- hisani)

Kichapo hicho kimezidisha shinikizo la kutimuliwa kwa mkufunzi Ole Gunner.

Kwingineko Manchester City waliwashinda Burnely 2-0 huku vijana wake Thomas Tuchel Chelsea wakiendeleza matokeo mazuri kwa kuwafunga limbukeni Brentford 1-0 na kuzidi kileleni mwa ligi kuu.

Totenham Hotspurs waliwapigisha magoti Newcastle 3-2 ugani St James Park mbele ya wamiliki wapya.

Jinsi K’ogalo ilivyoibamiza Al-Ahly ya Sudan


Na FK Zack

Miamba wa soka nchini Gor Mahia almaarufu K’ogalo walipata ushindi muhimu ugenini walipoirindima Al-Ahly Merowe ya Sudan 3-1 katika michuano ya CAF Confederation Cup wakisaka nafasi ya kushiriki katika mechi za makundi.

Wenyeji Al-Ahly walitangulia kuliona lango la Gor dakika tatu kupitia kwa Ahmed Abok.

Katika kipindi cha pili, K’ogalo ilirejea kwa makali na kuanza kumiliki mpira na katika dakika ya 55′, Samuel Onyango alifunga kupitia mkiki wa penalti. 

Wachezaji wa Gor Mahia. (Picha– hisani)

Gor Mahia ilizidisha mashambulizi na baada ya sakasaka Benson Omala alifunga la pili dakika ya 65′ na kuwaweka uongozini.

Mashambulizi yalizidi huku Gor ikitafuta la tatu na, jinsi wasemavyo Waswahili atafutaye hachoki, Ulimwengu Jules alifunga dakika ya 70′. 

Ushindi huu unaiweka Gor guu moja katika makundi wakisubiri mechi ya marudio.

Qatar 2022: Usiku mrefu kwa Stars baada ya kichapo cha Mali


Kikosi cha Harambee Stars chini ya kocha Engin Firat hapo jana kilipata kichapo cha mabao 5-0 kutoka kwa Mali katika mechi za kusaka nafasi ya kuwakilisha Kenya katika kombe la dunia.

Mabao yake Ibarahima Kone (3) na Adama Traore (1) katika kipindi cha kwanza yaliwachanganya na kuwapoteza Harambee Stars mchezoni, mwishowe Farouk Shikhalo akijifunga.

Kenya ilianza vyema dakika ya kwanza baada ya Micheal Olunga kupokea pasi safi kutoka kwa Aboud Omar lakini akalikosa lango kwa inchi kadhaa.

Dakika ya 8′ ndipo karamu na kichapo cha mabao kilianza baada ya Joash Onyango, ambaye kwa mara ya kwanza alikua anacheza kama beki wa kulia nafasi ambayo hajazoea, alipitwa na pasi ikamfikia Adama Traore na kufunga bila wasiwasi.

Mchezaji wa Harambee Stars na mpira. Picha | Hisani

Dakika ya 22′ Kone alifunga la Pili baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Charles Traore. Ilibidi kocha afanye mabadiliko kwa kuwa safu ya ulinzi haikuwa imara, Abdallah Hassan akaingia mahali pake Joash Onyango naye Zakayo Erick akaingia nafasi yake Lawrence Juma.

Mabadaliko hayo hayakusaidia sana na dakika ya 36′ Kone alifunga la pili. Mali ikiendelea na ushambulizi na hatimaye Moussa Djenepo aliangusha na Abdallah Hassan katika kisanduku na wakazawadiwa penalti, Kone hakusita kufunga lake la tatu na kufanya mambo kuwa 4 – 0 wakienda katika mapumziko.

Katika kipindi cha pili, Mali ilimiliki mpira na hatimaye kusababisha Farouk Shikhalo kujifunga.

Mali ilipata ushindi muhimu (5-0) na kuwa kileleni mwa kundi nayo Kenya ya tatu na alama mbili, alama tatu nyuma ya Uganda walioshinda mechi ya awali kati yao na Rwanda.

Qatar 2022: Kenya kukabiliana na Mali chini ya kocha mpya


Na FK Zack

Baada ya mechi za ligi tofauti duniani kuchezwa wikendi iliyopita, macho yote yanaangazia mechi za kimataifa huku mataifa mbalimbali yakisaka tiketi ya kushiriki kombe la dunia huko Qatar. 

Kenya  haijawachwa nyuma huku ikisafiri kuenda kutafuta ushindi wao wa kwanza  watakapo kutana na Mali huko Morocco.

Kenya ipo katika kundi moja na Uganda, Rwanda na Mali, na inashikilia nambari mbili katika kundi hilo baada ya kutoka sare mbili dhidi ya Rwanda na Uganda. 

Mengi yamejiri katika kandanda ya Kenya, habari kuu ikiwa kufutwa kazi kwa aliyekuwa kocha mkuu Ghost Mulee na kisha Engin Firat kuchukua mikoba yake.

Stars wanajiandaa kukabiliana na Mali kesho. Picha- Hisani

Engin alikitaja kikosi cha mwisho Jumatatu ambacho kilisafiri kuelekea Morocco kwa mechi ya Jumatano. 
Kikosi hicho kinashabikiwa kwa kuwa safari hii kocha ameweza kuchanganya wachezaji wakongwe na wale wachanga na kinatazamiwa kuleta upinzano unaostahili katika mechi ijayo.

Mechi hio itachezwa kule Morocco kwa kuwa Mali haina viwanja ambavyo vinafikia viwango vya Fifa. Inatazamiwa kuwa ngumu ukizingatia Mali ipo katika viwango bora kuliko Kenya katika takwimu za kimatifa za Fifa.