Category Archives: Lugari Sports Journal

A meaningful collection of sports events from Lugari and the world.

Jinsi K’ogalo ilivyoibamiza Al-Ahly ya Sudan


Na FK Zack

Miamba wa soka nchini Gor Mahia almaarufu K’ogalo walipata ushindi muhimu ugenini walipoirindima Al-Ahly Merowe ya Sudan 3-1 katika michuano ya CAF Confederation Cup wakisaka nafasi ya kushiriki katika mechi za makundi.

Wenyeji Al-Ahly walitangulia kuliona lango la Gor dakika tatu kupitia kwa Ahmed Abok.

Katika kipindi cha pili, K’ogalo ilirejea kwa makali na kuanza kumiliki mpira na katika dakika ya 55′, Samuel Onyango alifunga kupitia mkiki wa penalti. 

Wachezaji wa Gor Mahia. (Picha– hisani)

Gor Mahia ilizidisha mashambulizi na baada ya sakasaka Benson Omala alifunga la pili dakika ya 65′ na kuwaweka uongozini.

Mashambulizi yalizidi huku Gor ikitafuta la tatu na, jinsi wasemavyo Waswahili atafutaye hachoki, Ulimwengu Jules alifunga dakika ya 70′. 

Ushindi huu unaiweka Gor guu moja katika makundi wakisubiri mechi ya marudio.

Qatar 2022: Usiku mrefu kwa Stars baada ya kichapo cha Mali


Kikosi cha Harambee Stars chini ya kocha Engin Firat hapo jana kilipata kichapo cha mabao 5-0 kutoka kwa Mali katika mechi za kusaka nafasi ya kuwakilisha Kenya katika kombe la dunia.

Mabao yake Ibarahima Kone (3) na Adama Traore (1) katika kipindi cha kwanza yaliwachanganya na kuwapoteza Harambee Stars mchezoni, mwishowe Farouk Shikhalo akijifunga.

Kenya ilianza vyema dakika ya kwanza baada ya Micheal Olunga kupokea pasi safi kutoka kwa Aboud Omar lakini akalikosa lango kwa inchi kadhaa.

Dakika ya 8′ ndipo karamu na kichapo cha mabao kilianza baada ya Joash Onyango, ambaye kwa mara ya kwanza alikua anacheza kama beki wa kulia nafasi ambayo hajazoea, alipitwa na pasi ikamfikia Adama Traore na kufunga bila wasiwasi.

Mchezaji wa Harambee Stars na mpira. Picha | Hisani

Dakika ya 22′ Kone alifunga la Pili baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Charles Traore. Ilibidi kocha afanye mabadiliko kwa kuwa safu ya ulinzi haikuwa imara, Abdallah Hassan akaingia mahali pake Joash Onyango naye Zakayo Erick akaingia nafasi yake Lawrence Juma.

Mabadaliko hayo hayakusaidia sana na dakika ya 36′ Kone alifunga la pili. Mali ikiendelea na ushambulizi na hatimaye Moussa Djenepo aliangusha na Abdallah Hassan katika kisanduku na wakazawadiwa penalti, Kone hakusita kufunga lake la tatu na kufanya mambo kuwa 4 – 0 wakienda katika mapumziko.

Katika kipindi cha pili, Mali ilimiliki mpira na hatimaye kusababisha Farouk Shikhalo kujifunga.

Mali ilipata ushindi muhimu (5-0) na kuwa kileleni mwa kundi nayo Kenya ya tatu na alama mbili, alama tatu nyuma ya Uganda walioshinda mechi ya awali kati yao na Rwanda.

Qatar 2022: Kenya kukabiliana na Mali chini ya kocha mpya


Na FK Zack

Baada ya mechi za ligi tofauti duniani kuchezwa wikendi iliyopita, macho yote yanaangazia mechi za kimataifa huku mataifa mbalimbali yakisaka tiketi ya kushiriki kombe la dunia huko Qatar. 

Kenya  haijawachwa nyuma huku ikisafiri kuenda kutafuta ushindi wao wa kwanza  watakapo kutana na Mali huko Morocco.

Kenya ipo katika kundi moja na Uganda, Rwanda na Mali, na inashikilia nambari mbili katika kundi hilo baada ya kutoka sare mbili dhidi ya Rwanda na Uganda. 

Mengi yamejiri katika kandanda ya Kenya, habari kuu ikiwa kufutwa kazi kwa aliyekuwa kocha mkuu Ghost Mulee na kisha Engin Firat kuchukua mikoba yake.

Stars wanajiandaa kukabiliana na Mali kesho. Picha- Hisani

Engin alikitaja kikosi cha mwisho Jumatatu ambacho kilisafiri kuelekea Morocco kwa mechi ya Jumatano. 
Kikosi hicho kinashabikiwa kwa kuwa safari hii kocha ameweza kuchanganya wachezaji wakongwe na wale wachanga na kinatazamiwa kuleta upinzano unaostahili katika mechi ijayo.

Mechi hio itachezwa kule Morocco kwa kuwa Mali haina viwanja ambavyo vinafikia viwango vya Fifa. Inatazamiwa kuwa ngumu ukizingatia Mali ipo katika viwango bora kuliko Kenya katika takwimu za kimatifa za Fifa.

UCL: Liverpool yang’aa Porto huku City ikijutia PSG


• Na FK Zack

Mechi za makundi katika kipute cha ligi ya mabingwa (UCL) ziliendelea hapo jana. Jumla ya ngaramba nane zilichezwa katika viwanja tofauti tofauti. 

PSG yaikung’uta City

Mchezaji nyota Lionel Messi (katikati) akiwaongoza PSG kusherehekea ushindi dhidi ya City. Picha– hisani

Mechi iliyokuwa imesubiriwa kwa hamu ni kati ya mabingwa mara 9 wa Ligue 1 PSG na mabingwa mara tano wa kombe la EPL Manchester City, PSG wakipata ushindi muhimu 2-0. 


Mechi ilianza kwa kasi huku timu zote mbili zikifanya shambulizi baada ya shambulizi. PSG  waliweza kushambulia dakika ya 8′ na wakapata bao  kupitia kwa mchezaji Idrissa Gueye na kuiweka kileleni hadi kipindi cha kwanza kukamilika. 


Kipindi cha pili, City walizidisha mihemko lakini hawakufanikiwa kupata nafasi ya kusawazisha. Lionel Messi alizamisha matumaini ya City kupata angalau sare katika mechi hii alipofunga bao lake la kwanza tangu ajiunge na miamba hawa wa Ufaransa kutoka Barcelona.


Liverpool yainyamazisha Porto

Nyota wa Liverpool na Misri Mohamed Salah (kushoto) na mwenzake Virgil Dijk wakifurahia mwelekeo wa mchezo. Picha– hisani

Mabingwa mara 6 wa kombe la mabingwa Liverpool waliweza kuwanyamazisha Porto kwao nyumbani walipowalaza  mabao matano kwa moja (5-1).

 

Mohamed Salah na Roberto Firmino walifunga mawili kila mmoja naye Sadio Mane akafunga moja.


Porto walipata zilizochezwa:achozi kupitia kwa Mehdi Taremi. 


Matokeo jumla ya mechi zilizochezwa: