Tag Archives: Michezo

Sports Roundup: Matukio muhimu viwanjani wikendi


Na Tom Lutali

Wikendi hii imeshuhudiwa matukio mbalimbali kutoka riadha hadi kandanda.

Wakenya wang’aa katika riadha

Kwenye mashindano yanayoendelea ya Africa Duathtop Championship nchini Namibia upande wa akina dada, Mkenya Yvonne Zilpa alishinda nishani ya dhahabu .

Upande wa wanaume, Elisha Rotich alimaliza wa kwanza Kwa muda wa dakika 2:04:18 na kuandikisha muda bora wake wa binafsi. Kariuki Mungai alimaliza wa tatu.

Wanariadha wa Kenya waling’aa wikendi hii. (Picha- hisani)

United yapata kichapo huku Liverpool na Chelsea ziking’aa

Miamba wa Anfield Liverpool waliwaadhibu Watford 5-0 na kuendeleza rekodi yake ya kutoshindwa msimu huu.

Kwingineko, masaibu ya mashetani wakendu Manchester Unitedyaliendelea Jumamosi ugani Kingpower baada ya kufungwa 4-2 na Leicester City.

Mohamed Salah akiwaongoza wenzake kusherehekea ushindi wa Liverpool. (Picha- hisani)

Kichapo hicho kimezidisha shinikizo la kutimuliwa kwa mkufunzi Ole Gunner.

Kwingineko Manchester City waliwashinda Burnely 2-0 huku vijana wake Thomas Tuchel Chelsea wakiendeleza matokeo mazuri kwa kuwafunga limbukeni Brentford 1-0 na kuzidi kileleni mwa ligi kuu.

Totenham Hotspurs waliwapigisha magoti Newcastle 3-2 ugani St James Park mbele ya wamiliki wapya.

Jinsi K’ogalo ilivyoibamiza Al-Ahly ya Sudan


Na FK Zack

Miamba wa soka nchini Gor Mahia almaarufu K’ogalo walipata ushindi muhimu ugenini walipoirindima Al-Ahly Merowe ya Sudan 3-1 katika michuano ya CAF Confederation Cup wakisaka nafasi ya kushiriki katika mechi za makundi.

Wenyeji Al-Ahly walitangulia kuliona lango la Gor dakika tatu kupitia kwa Ahmed Abok.

Katika kipindi cha pili, K’ogalo ilirejea kwa makali na kuanza kumiliki mpira na katika dakika ya 55′, Samuel Onyango alifunga kupitia mkiki wa penalti. 

Wachezaji wa Gor Mahia. (Picha– hisani)

Gor Mahia ilizidisha mashambulizi na baada ya sakasaka Benson Omala alifunga la pili dakika ya 65′ na kuwaweka uongozini.

Mashambulizi yalizidi huku Gor ikitafuta la tatu na, jinsi wasemavyo Waswahili atafutaye hachoki, Ulimwengu Jules alifunga dakika ya 70′. 

Ushindi huu unaiweka Gor guu moja katika makundi wakisubiri mechi ya marudio.

Qatar 2022: Kenya kukabiliana na Mali chini ya kocha mpya


Na FK Zack

Baada ya mechi za ligi tofauti duniani kuchezwa wikendi iliyopita, macho yote yanaangazia mechi za kimataifa huku mataifa mbalimbali yakisaka tiketi ya kushiriki kombe la dunia huko Qatar. 

Kenya  haijawachwa nyuma huku ikisafiri kuenda kutafuta ushindi wao wa kwanza  watakapo kutana na Mali huko Morocco.

Kenya ipo katika kundi moja na Uganda, Rwanda na Mali, na inashikilia nambari mbili katika kundi hilo baada ya kutoka sare mbili dhidi ya Rwanda na Uganda. 

Mengi yamejiri katika kandanda ya Kenya, habari kuu ikiwa kufutwa kazi kwa aliyekuwa kocha mkuu Ghost Mulee na kisha Engin Firat kuchukua mikoba yake.

Stars wanajiandaa kukabiliana na Mali kesho. Picha- Hisani

Engin alikitaja kikosi cha mwisho Jumatatu ambacho kilisafiri kuelekea Morocco kwa mechi ya Jumatano. 
Kikosi hicho kinashabikiwa kwa kuwa safari hii kocha ameweza kuchanganya wachezaji wakongwe na wale wachanga na kinatazamiwa kuleta upinzano unaostahili katika mechi ijayo.

Mechi hio itachezwa kule Morocco kwa kuwa Mali haina viwanja ambavyo vinafikia viwango vya Fifa. Inatazamiwa kuwa ngumu ukizingatia Mali ipo katika viwango bora kuliko Kenya katika takwimu za kimatifa za Fifa.

Ratiba ya UCL: Mabingwa watetezi Chelsea kukabili Juventus


Na Tom Lutali

Chelsea watakuwa wageni wa Juventus usiku wa leo katika kipute cha kuwania kombe la klabu bingwa Uropa (UCL).

Mabingwa hao watetezi wanapania kujikwamua baada ya kufungwa Jumamosi na Manchester City 1-0 kwo Stamford Bridge katika ngaramba ya EPL.
Juventus, kwa upande wao, wanataka kuendeleza msusuru wa matokeo mazuri maana watakuwa wanatafuta ushindi wao wa tano katika michuano yao yote msimu huu.
Chelsea watakuwa bila kiungo wao muhimu raia wa Ufaranza NG’olo Kante ambaye anaugua.
Juventus nao hawatakuwa na mashambuliaji wao matata Alvaro Morota na Paulo Dybala ambao wanauguza majeraha.

Ratiba ya leo katika UCL
• Atalanta vs Young Boys– 19:45
• Zenit vs Malmo– 19:45
• Bayern Munich vs Dynamo Kyiv– 22:00
• RB Salzburg vs Lille– 22:00
• Juventus vs Chelsea– 22:00
• Manchester United vs Villarreal– 22:00