Philip Etale atangaza kuambukizwa Covid-19 kwa mara ya pili


• Na Tom Lutali

Mkuu wa mawasiliano katika chama cha ODM Philip Etale ametangaza kuathirika na virusi vya Covid-19 kwa mara ya pili sasa.

Etale amesema kuwa tangu Jumatatu wiki iliyopita, mwili wake umekuwa ukiashiria dalili ambazo si za kawaida kama vile kukohoa, kuumwa kichwa na pua yake kubana.

Mwanzoni alidhani kuwa ni homa tu ya kawaida lakini akazidiwa na kuamua kutafuta huduma za matibabu. Alijaribu kununua dawa dukani lakini hakupata nafuu.

Mkuu wa mawasiliano katika ODM Philip Etale ametangaza kuwa ameambukizwa Covid-19 kwa mara ya pili tena. Picha– Hisani

Kupitia ukrasa wake wa Facebook, Etale amesema alitembelea hospitali kuu ya Agha Khan, Nairobi, ambapo alipimwa na kupatikana na virusi vya Corona.

Etale, ambaye ametaja hali yake kuwa ya matumaini, ameomba kujitenga na mitandao ya kijamii kwa muda huku akirai wananchi kuwa makini kwa kuwa wimbi jipya la Covid-19 ‘si mchezo’.

1 thought on “Philip Etale atangaza kuambukizwa Covid-19 kwa mara ya pili

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.