Category Archives: Newspaper Review

A comprehensive perusal inside leading national and international dailies.

Magazetini Jumatano: Kenya yapinga uamuzi kuhusu mpaka na Somalia


Na Collins Oluyali

Magazeti ya Jumatano yana taarifa kuhusu masaibu yanayokumba chama cha Jubilee kinachoongozwa na rais Uhuru Kenyatta.

Magazeti haya pia yana taarifa kuhusu uamuzi wa mahakama ya ICJ kuhusu mzozo wa mpaka kati ya Kenya na Somalia.

People Daily

Mahakama ya Umoja wa Mataifa (UN) ilitoa uamuzi wake kwenye mzozo wa mpaka kati ya Kenya na Somalia baada ya kikao cha majaji huko Hague.

Somalia ilishinda kesi hiyo na sasa Kenya huenda ikapoteza kilomita kadhaa kwenye bahari katika mpaka wake na Somalia.

Somalia ndiyo ilifika kwenye mahakama hiyo mwaka wa 2014 baada ya kudai Kenya imenyakua sehemu yake.

Ni uamuzi ambao tayari umemkera rais Uhuru Kenyatta na kusema Kenya haiwezi kukubaliana nao.

Katika uamuzi wake, mahakama iligawa sehemu yenye utata mara mbili na Somalia inadaiwa kufaidika pakubwa na sehemu iliyo na ukwasi wa mafuta na samaki.

The Star

Mhariri wa The Star imeipa kipau mbele taarifa kuhusu chama cha Jubilee ambacho kimekumbwa na masaibu na sasa kinapanga kuwafuta kazi maafisa wake kadhaa.

Jubilee imekuwa ikiisha makali tangu mzozo wa uongozi uibuke kati ya kambi zinazoegemea upande wa rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto.

Magazetini Jumatatu: Wanaopigiwa debe kumrithi Uhuru kutoka Mlima Kenya


Na Collins Oluyali

Magazeti ya Jumatatu yanagusia shughuli kabambe katika eneo lenye ukwasi wa kura la Mlima Kenya huku wagombeaji wakuu wa urais wakiendelea kukita kambi eneo hilo kuwinda kura.

Magazeti haya pia yanaripoti kupungua kwa umaarufu wa rais Uhuru Kenyatta katika eneo hilo.

The Standard

Kulingana na gazeti hili, eneo la Mlima Kenya halitawaunga mkono wagombeaji waliokita kambi eneo hilo wakitaka kumrithi Uhuru ambaye anakaribia kustaafu.

Kwa muda mrefu sasa, wagombeaji wakuu wa urais 2022 wamekuwa wakikita kambi katika eneo hilo kutafuta uungwaji mkono.

Kumekuwa na dhana kuwa hakuna kiongozi kutoka eneo hilo aliyetosha kwa sasa kuchukua kiti hicho kutoka kwa Uhuru.

The Standard limeangazia misingi ambayo eneo hilo litatumia kuwafungia wagombea wa nje na kumuunga mkono mgombea wao katika uchaguzi mkuu ujao.

Huku wakfu wa wafanyibiashara kutoka Mlima Kenya wa Mount Kenya Foundation ukiahidi kuunga mkono mgombea wa upinzani, bado kundi hilo linaweza kumshawishi mgombea wao kumrithi Uhuru.

Miongoni mwa wale waliopendekezwa ni Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi, na kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua.

Mt Kenya inajivunia jumla ya wapiga kura milioni 7 na linalenga kuwasajili wapiga kura milioni 9 katika zoezi linaloendelea.

Daily Nation

Kulingana na gazeti hili, Uhuru yuko njia panda huku macho yote yakielekezwa kwake akitarajiwa kumtaja mrithi wake 2022.

Rais amekuwa akisema kuwa atawacha taifa hili katika mikono salama bila kutaja ni nani atakuwa mrithi wake.

Wandani wa karibu wa Uhuru wamekuwa wakidokeza kuwa kiongozi wa ODM Raila Odinga ambaye alikiri anajifunza kukwea mlima.

Lakini bado rais hajataja anamuunga nani mkono kuwa mrithi wake.

Hata hivyo, wanasiasa wa Mt Kenya wanaomuegemea naibu rais William Ruto wamemuomba asusie siasa za urithi na kuwacha eneo hilo kuchagua kiongozi wao bila kushawishika.

Je, una taarifa muhimu ungependa ichapishwe na Lugari Daily? Wasiliana nasi katika barua pepe lugaridaily@gmail.com.

Magazetini Jumatatu: Ruto afunguka kuhusu kufeli kwa maridhiano na rais


• Na Tom Lutali

Magazeti ya Jumatatu, Oktoba 4 yanaangazia kugonga mwamba kwa wito wa kuwapatanisha rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto ambao ulipendekezwa na Muungano wa Maaskofu wa Kanisa Katoliki (KCCB).
Magazeti haya pia yamegusia Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuanzisha zoezi la kusajili wapiga kura.

Daily Nation
Daily Nation linaripoti kuwa Ruto amejiondolea lawama katika kushindikana upatanisho kati yake na Uhuru kama ilivyokuwa imependekezwa na maaskofu wa kanisa Katoliki.

Mnamo Septemba, sehemu ya maaskofu wa kanisa Katoliki walikuwa wamewaomba viongozi hao wawili kuzungumza na kuzika uhasama kati yao.
Ruto alikubali wito huo lakini Ikulu ya Nairobi ilisalia bubu kuhusu suala hilo.
Katika taarifa rasmi iliyotolewa Septemba 26 kwa maaskofu hao, Ruto alisema alikuwa tayari kupatanishwa na bosi wake lakini upande mwingine ulidinda.
Ruto alitoa ushahidi wake kuonyesha alikubali wito wa maaskofu wa kanisa katoliki kumpatanisha na rais.
“Ninashukuru sana na kukubali kwa unyenyekevu kuwa uhusiano wangu na rais umekuwa suala la kuwapa wasiwasi kuhusiana na umoja humu nchini. Nataka niwahakikishie kuwa mimi sina lolote kumhusu rais,” ilisoma barua ya Ruto.

The Standard

Gazeti hili pia limegusia kizingiti katika upatanisho kati ya rais na naibu wake.
Huku Ruto akionekana kuwa tayari kupatanishwa, upande wa Uhuru unaonyesha kuwa kizingiti na kukataa kujibu ombi la maaskofu Wakatoliki.
Hata hivyo, wanasiasa wanaomuegemea Uhuru wamejitokeza kumtetea rais kuhusu suala hilo.
Mwishoni mwa Septemba, Mbunge wa Nyeri Mjini Wambugu Ngunjiri alipuzilia mbali pendezo la maaskofu hao akitaja kutokuwa na uaminifu.
Wambugu alielekezea kidole cha lawama kanisa akidai lilichangia katika uhasama wa viongozi hao.
Kulingana na mbunge huyo, hii ni kutokana na wanasiasa kugeuza kanisa kuwa uwanja wa kueneza siasa ambapo huwa wanashambuliana mbele ya viongozi wa kanisa.
Alishangaa mbona maaskofu hao walisalia kimya kwa muda mrefu na kuwataka kubeba msalaba wao kabla ya kupendekeza utangamano.


Ad

Magazetini Jumanne: Ruto kujipanga upya Raila akizidi kukweya Mlima 


Na Collins Oluyali

Magazeti ya Jumatano yanaendelea kuangazia juhudi za kinara wa ODM Raila Odinga kutafuta uungwaji mkono wa eneo la Mlima Kenya katika safari yake ya kuingia Ikulu 2022.

People Daily
Siku moja tu baada ya kinara wa ODM kufanya ziara katika eneo la Mlima Kenya na kuhubiri ajenda yake kwa eneo hilo, sasa amefanya kikao na wafanyabiashara sugu kutoka Mlimani.

Raila alikuwa katika mkahawa wa Safari Park ambapo alikutana na mabwanyenye hao wakiongozwa na mwenyekiti wa benki ya Equity Peter Munga.

Chini ya mwavuli wa Mt Kenya Foundation, Raila alipata nafasi ya kuuza sera zake kwa kikao hicho.

Baadhi ya wanachama wa vuguvugu hilo ni mjomba wake rais Uhuru Kenyatta, George Muhoho, SK Macharia wa RMS, mkurugenzi wa KenGen Eddy Njoroge na wengine.

The Star
Gazeti hili pia linaangazia siasa za 2022 ambapo naibu rais William Ruto na kinara wa ODM Raila Odinga wanajikakamua kucheza kadi zao.

Jarida hili linasema DP Ruto anaonekana kubadili mwelekeo wa siasa zake na sasa ameachana na ajenda ya hustlers vs dynasties.

Aidha, inaarifiwa kuwa ametafuta kundi lingine na washauri ili kumsaidia kukwea Mlima wa kuingia Ikulu 2022.

Daily Nation
Gazeti la Nation lina taarifa kuhusu kurejea kwa aliyekuwa mkurugenzi wa tume huru ya mipaka na uchaguzi nchini IEBC Ezra Chiloba.

Chiloba sasa ameteuliwa kujiunga na tume ya mawisiliano nchini CAK.

The Standard
Gazeti la Standard linasema rais Uhuru Kenyatta amewapa wanachama wa Mt Kenya Foundation wajibu wa kumtafuta kigogo atakayeungwa mkono na eneo la Mlima Kenya katika uchaguzi wa urais 2022.

Kundi hilo liliketi na Raila Odinga Jumanne Septemba 28 na sasa inaarifiwa Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi na Gideon Moi pamoja na Moses Wetangula watahudhuria kikao chao Ijumaa Sepetmba 30.

Naibu Rais William Hata hivyo ametengwa na wanasema hawatamuita kuuza sera zake.