Magazetini Jumatatu: Uhuru, Raila wanapanga muungano kama Narc


Na Collins Oluyali

Magazeti ya leo yanaangazia pakubwa siasa za 2022 huku upande wa upinzani ukibuni mikakati kabambe ya kutwaa ushindi.

Magazeti haya pia yanaripoti kuhusu ukaguzi wa mali ya maafisa wa serikali huku Seneti ikipanga kujadili mswada huo.

Daily Nation

Kulingana na gazeti hili, rais Uhuru Kenyatta na mwenzake wa kinara wa ODM Raila Odinga wako kwenye mpango wa kubuni mrengo wa kisiasa utakaotumika katika uchaguzi wa urais wa 2022.

Wawili hao watatumia wazo la mrengo wa Rainbow ambao rais mstaafu Mwai Kibaki alitumia kutwaa mamlaka 2002.

Mrengo huo unapania kuzima ushawishi wa naibu rais Willam Ruto ambaye anaonekana kuwa tishio kwenye mbio hizo za kuwania urais.

Chama tawala cha Jubilee na upinzani ODM vinafanya mazungumzo ya kuhakikisha wanashinda kiti cha urais.

Vyama hivyo, katika kampeni zao, vinalenga mambo matatu yaliyotumiwa na Narc mwaka 2002, ambayo wanatumainia yatakuwa ya maana katika uchaguzi ujao.

The Standard

Katika gazeti hili, Ruto alianza kampeni baada ya serikali ya Jubilee kumtema.

Katika kampeni zake za miaka miwili, Ruto ameweza kuteka maeneo ambayo yana ukwasi wa kura hususan Mlima Kenya.

Kampeni zake zimekuwa zikimuweka kifuambele dhidi ya mahasidi wake wanaomezea mate kiti cha urais.

Hata hivyo, bahati ya Ruto inaonekana kudidimia baada ya hasidi wake mkubwa Raila kuanzisha kampeni ya ‘Azimio La Umoja’ ambazo zimekuwa zikiwavizia wapiga kura.

Kampeni za Raila zimeonekana kuzima juhudi za Ruto.

Kutokana na hayo, The Standard inashangaa iwapo Ruto atakuwa akiongoza mbio ama kuwa mdhibiti wa mbio.

Lakini Ruto anaonekana kutokata tamaa huku akivamia ngome za Raila hivi majuzi akizuru eneo la Pwani.
People Daily
Mswada mpya umewasilishwa katika Bunge la Seneti ambao utawalazimu maafisa wa serikali na jamaa zao mali zao kukaguliwa.

People Daily

Mswada mpya umewasilishwa katika Bunge la Seneti ambao utawalazimu maafisa wa serikali na jamaa zao mali zao kukaguliwa.

Mswada huo kwa sasa upo kwenye hatua ya pili na unatarajiwa kujadiliwa Jumanne, Oktoba 19.

Iwapo mswada huo utapitishwa, maafisa wote wa serikali, akiwemo rais na naibu wake, ni lazima mali zao zitakaguliwa na kuwekwa wazi.

Taifa Leo

Taifa Leo linaripoti kuwa vijana wanawakaidi wazee katika chaguo lao kuelekea chaguzi za 2022.

Wazee katika maeneo tofauti wamekuwa wakitoa kauli zao kuhusu ni nani wanapendelea kuwa rais.

Kwa mfano katika baraza la wazee la Muyoot la Kalenjin limegawanyika katika kumchagua Ruto.

Katika eneo la kati mwa Kenya, mgawanyiko huo umekuwa ukishuhudiwa huku wakiwateua wagombeaji wao.

Baadhi yao wamemteua Spika Justin Muturi, wengine wakimuunga mkono Ruto wengine wakimuegemea kinara wa ODM Raila Odinga.

The Star

Raila atarejea katika eneo la Mlima Kenya kutafuta uungwaji mkono.

Kinara wa ODM atatua katika kaunti za Tharaka Nithi, Meru na Embu.

Raila atapokelewa na magavana watatu Muthomi Njuki (Tharaka Nithi), Kiraitu Murungi (Meru) na Martin Wambora(Embu) .

Waziri wa Kilimo Peter Munya pia anatazamiwa kuandamana na Raila wakati wa ziara hiyo.

Hata hivyo, kuna uwezekano Munya atasusia mkutano huo sababu ya uhasama wake na Kiraitu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.