‘Kutokubali kuachwa na mpenzi ni hatari kuliko Corona’


Na Hosea Namachanja

“Kukua mkubwa si kwa kimo, umri au kututumua mwili. Kukua kifikra ni kukubali kuachwa na mpenzi na kusonga mbele kimaisha. Lakini kutokubali kuachwa au kusalitiwa, ni ugonjwa hatari kuliko Corona,” Dkt. Joshua ausia wanachuo wa Moi siku ya Jumamosi kwenye ukumbi wa Conference Room, kwenye maktaba ya Moi.

Haya ni baada ya kuwapo kwa kongamano la siku tatu la Mental Health Awareness lililonuwia kuwausia, elimisha na kuzuia maenezi na chimbuko la vifo vya mapema miongoni mwa vijana .

Suala la mahusiano likipigiwa upato na matumizi ya mihadarati, Dkt. Carolyne, ambaye ni mwanasaikolojia kutoka Hope Well asema kuwa ni vyema vijana kuepukana na masuala ya mahusiano, shinikizo la rika, matumizi ya mihadarati na kujali afya yao.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Moi wakihudhuria maadhimisho ya siku ya afya ya kiakili duniani. (Picha– Hosea Namachanja)

“Mwaka jana na huu mwaka, umri mdogo ambao nimekabiliana nao kazini unaosumbuliwa na matatizo ya kiafya na akili ni miaka tisa na 79. Hii ina maana kuwa Mental Health issue si tatizo linalobagua,” Asema Dkt. Carolyne.

Aongezea kuwa, “Ni vyema vijana kujizatiti kuepukana na vitu ambavyo vinawazulia matatizo ya kiafya na kiakili. Pia, asisitiza kuwa, kuridhika na kile ambacho mzazi amekutumia ni njia mojawapo ya kuzuia matatizo ya kiakili na kiafya.”

Lakini, je, kampeni hii ya kuzuia vifo vya mapema miongoni mwa vijana na watu wazima itafaulu? Mheshimiwa Collins Kemboi asema kuwa usalama unaanza na sisi wenyewe– kujilinda, kujali rafiki zetu na jamaa zetu.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Moi wakihudhuria maadhimisho ya siku ya afya ya kiakili duniani. (Picha– Hosea Namachanja)

“Ukimwona mwenzako asumbuliwa na tatizo labda la mahitaji ya kawaida kama vile chakula, usimwache aumie. Mwokoe mwenzako. Nawe mwenyewe ukisalitiwa na mpenzi wako, dadangu na kakangu, kubali kuachika. Kuachwa kwingine huwa ukombozi wa mateka na upofu wa mapenzi yasiyo na mafanikio.”

“Kunywa sumu au kujitia kitanzi na kujinyonga hadi kufa si mwisho wa maisha na si rahisi. Kuna machungu pia. Hamna kifo kitamu. Mbona uzulie familia yako au rafiki zako msongo wa mawazo ambao pia ni tatizo la kiafya na kiakili ilhali dawa mjaarabu ipo? Ongea usikike. Piga unyende uokolewe na omba wosia, uusiwe.” Aongezea mheshimiwa.

Naye Kiranja mkuu wa wanachuo kitengo cha Social Welfare Bi Glory Kathure apigia upato kuwa, vijana wasisingizie uwepo wa Corona kama chanzo pekee cha matatizo ya kiakili na kiafya. Wanachuo wachukue chanjo dhidi ya virusi vya Corona kuzuia maambukizi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.