Magazetini Ijumaa: Ruto anapoteza umaarufu Mlima Kenya


Na Collins Oluyali

Magazeti ya Ijumaa yanaangazia taarifa kadhaa ikiwemo ubabe wa kisiasa kati ya naibu rais William Ruto na kinara wa ODM Raila Odinga eneo la Mlima Kenya.

Kuna taarifa pia kuhusu mauaji ya mwanariadha Agnes Tirop ambaye alipatikana amedungwa kisu katika kile kinaaminika kuwa mzozo wa kimapenzi.

The Star

The Star imefanya utafiti kutathmini mgombea wa urais aliye maarufu zaidi katika eneo la Mlima Kenya.

Utafiti huo unaonyesha Ruto angali ana wafuasi wengi eneo hilo baada ya kuzoa asilimia 57 ya waliohojiwa.

Asilimia 11 wanaunga mkono kinara wa ODM Raila Odinga.

Hata hivyo, utafiti huo unaonyesha umaarufu wa DP unashuka tangu Raila aanze kampeni katika eneo hilo.

People Daily

Taarifa kuu hapa ni kuhusu Raila Odinga ambaye anaonekana kupata nguvu mpya katika safari ya kuelekea Ikulu.

Raila ameanza mikakati mipya ikiwemo kukutana na washikadau muhimu katika kutafuta kura za kutosha kumtangaza rais 2022.

Aidha ni wazi sasa kuwa serikali iko nyuma ya Raila, jambo ambalo linampa nguvu ya kuvuma kisiasa.

Kuna taarifa pia kuhusu kutupwa nje kwa kadi ya Huduma na mahakama ikisema sheria haikufuatwa.

Serikali ilitumia mabilioni ya fedha katika kuwasajili Wakenya lakini korti ilisema hakuna sheria ya kulinda deta za watu.
Standard

The Standard

Familia ya mwanariadha Agnes Tirop inaendelea kuomboleza kifo chake huku mamake akisema binti huyo aliwatembelea siku tatu zilizopita kabla ya kupatikana ameuawa.

“Tulikuwa nyumbani Jumapili Oktoba 10 na kisha akaondoka ili kuanza mazoezi yake kule Iten. Alikuwa ameleta karo ya ndugu zake watano kwa sababu shule zinafunguliwa,” mamake alisema.

Ametaka mkono wa serikali kuhakikisha kuwa familia yake inapata haki kwa kuwajibisha waliohusika.

“Nataka kujua ni kwa nini akamuua msichana ambaye amesaidia watu wengi hivi,” mamake alisema.

Tayari makachero wa DCI wamemtia mbaroni mumewe ambaye anadaiwa alihusika katika mauaji hayo.
Nation

Daily Nation

Jarida hili limezamia taarifa za mauaji ya Tirop ikiibuka mumewe alikuwa akimpa kichapo kwa mujibu wa dadake.

Kulingana na dadake, Tirop aligombana na mumewe siku ambaye alirejea nchini kutoka Tokyo na ilikuwa wazi kuwa ndoa yao ilikuwa na masaibu.

Aidha, licha ya mwili wake kupatikana Jumatano Oktoba 13, polisi wanachunguza iwapo huenda aliuawa Jumatatu usiku.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.