Magazetini Jumatatu: Wanaopigiwa debe kumrithi Uhuru kutoka Mlima Kenya


Na Collins Oluyali

Magazeti ya Jumatatu yanagusia shughuli kabambe katika eneo lenye ukwasi wa kura la Mlima Kenya huku wagombeaji wakuu wa urais wakiendelea kukita kambi eneo hilo kuwinda kura.

Magazeti haya pia yanaripoti kupungua kwa umaarufu wa rais Uhuru Kenyatta katika eneo hilo.

The Standard

Kulingana na gazeti hili, eneo la Mlima Kenya halitawaunga mkono wagombeaji waliokita kambi eneo hilo wakitaka kumrithi Uhuru ambaye anakaribia kustaafu.

Kwa muda mrefu sasa, wagombeaji wakuu wa urais 2022 wamekuwa wakikita kambi katika eneo hilo kutafuta uungwaji mkono.

Kumekuwa na dhana kuwa hakuna kiongozi kutoka eneo hilo aliyetosha kwa sasa kuchukua kiti hicho kutoka kwa Uhuru.

The Standard limeangazia misingi ambayo eneo hilo litatumia kuwafungia wagombea wa nje na kumuunga mkono mgombea wao katika uchaguzi mkuu ujao.

Huku wakfu wa wafanyibiashara kutoka Mlima Kenya wa Mount Kenya Foundation ukiahidi kuunga mkono mgombea wa upinzani, bado kundi hilo linaweza kumshawishi mgombea wao kumrithi Uhuru.

Miongoni mwa wale waliopendekezwa ni Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi, na kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua.

Mt Kenya inajivunia jumla ya wapiga kura milioni 7 na linalenga kuwasajili wapiga kura milioni 9 katika zoezi linaloendelea.

Daily Nation

Kulingana na gazeti hili, Uhuru yuko njia panda huku macho yote yakielekezwa kwake akitarajiwa kumtaja mrithi wake 2022.

Rais amekuwa akisema kuwa atawacha taifa hili katika mikono salama bila kutaja ni nani atakuwa mrithi wake.

Wandani wa karibu wa Uhuru wamekuwa wakidokeza kuwa kiongozi wa ODM Raila Odinga ambaye alikiri anajifunza kukwea mlima.

Lakini bado rais hajataja anamuunga nani mkono kuwa mrithi wake.

Hata hivyo, wanasiasa wa Mt Kenya wanaomuegemea naibu rais William Ruto wamemuomba asusie siasa za urithi na kuwacha eneo hilo kuchagua kiongozi wao bila kushawishika.

Je, una taarifa muhimu ungependa ichapishwe na Lugari Daily? Wasiliana nasi katika barua pepe lugaridaily@gmail.com.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.