Magazetini Jumanne Juni 15, 2021: Unahitaji digrii kugombea uchaguzi wa 2022– IEBC


• Na Collins Oluyali

Katika magazeti ya leo, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini (IEBC) imewaangushia wanasiasa shoka baada ya kutangaza kuwa yeyote anayepania kuwania wadhifa wowote wa uongozi katika uchaguzi wa 2022 lazima awe na shahada ya digrii kutoka chuo kikuu.

Magazeti haya pia yanaangazia tanzia ya Chris Kirubi, mwekezaji na mfanyibiashara tajika, aliyekumbana na mauti yake jana.

image

People Daily

Gazeti hili linaripoti kuwa mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amewakumbusha wanaopania kuwania viti vyovyote vya kisiasa kuwa sheria kuhusu chaguzi ibara ya 22 inasema ni lazima wagombeaji wawe na shahada kutoka kwa vyuo vikuu tajika ili kuwania viti katika chaguzi za 2022.

Kulingana na gazeti hili, kipengee hicho kinasema kuwa mgombea wa ubunge anaweza kuteuliwa kuwania uchaguzi endapo ana shahada kutoka chuo kikuu kinachotambulika Kenya.

Wanaowania kuwa wawakilishi wadi wanatakiwa kuwa na shahada kutoka kwa chuo kikuu tajika nchini. Chebukati alielezea kuwa tume yake inabuni Mkataba wa Makubaliano na Mamlaka ya Kitaifa ya Kuainisha Kufuzu kwa Asasi za Elimu ya Juu (KNQA) na Tume ya Elimu ya juu (CUE) kukagua shahada ambazo wagombeaji watawasilisha.

Lakini muungano wa mabunge ya kaunti (CAF) umeapa kufika kortini kukosoa sheria hiyo ukisema ni kinyume cha katiba.

The Star

Kulingana na The Star, rais Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa atamchagua mrithi wake wa mwaka 2022 miongoni mwa vinara wa Nasa endapo watakubaliana kumteua mgombea mmoja.

Tangazo hilo ni pigo kwa naibu rais William Ruto anayepania kumrithi Uhuru. Kwa mara ya kwanza, Uhuru aliwataka vinara wa Nasa kuungana pamoja ili kuimarisha nafasi yao ya kubuni serikali mpya baada ya kukamilika kwa muhula wake 2022.

Uhuru na Ruto wamekuwa na vita baridi wakati wa muhula wao wa pili mamlakani huku kiongozi wa taifa akionyesha ishara za kuvunjika kwa ndoa yao kisiasa.

image

The Standard

Gazeti hili limeangazia hatua za mwisho za mwanabiashara mashuhuri Chris Kirubi. Kulingana na The Standard, wengi walikuwa wanamtambua marehemu kama mtu tajiri lakini mwenye kiburi.

Gazeti hili limeripoti kuwa Kirubi alikuwa anapenda kumiliki vitu vya thamani maishani ikiwemo magari, suti na marashi, lakini alifariki akiwa mpweke Jumatatu, Juni 14.

Mfanyibiashara huyo aliangushwa na saratani nyumbani kwake ambapo alikuwa amejitengenezea chumba cha wagonjwa mahututi na kuzingiriwa na kikosi cha matabibu.

Daily Nation

Gazeti hili linaripoti kuhusu kifo cha Kirubi ambaye anajiunga na orodha ya watu mashuhuri waliomalizwa na ugonjwa wa saratani ikiwemo aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Safaricom Bob Collymore, mbunge wa Kibra Ken Okoth na gavana wa Bomet Joyce Laboso.

Daily Nation linaripoti kuwa Kirubi alikuwa amejipatia umaarufu wa kuwa mjasiriamali katika sekta ya habari, utengenezaji na kilimo-biashara.

Licha ya kufaulu kwake, Kirubi amekuwa akijipata taabani kufuatia kuporomoka kwa duka la Uchumi. Gazeti hili pia limegusia kifo cha aliyekuwa mbunge wa Gem, Jakoyo Midiwo.

Midiwo, aliyezaliwa 1966, alikuwa binamu wa kiongozi wa ODM Raila na Oburu Odinga.

Taifa Leo

Gazeti hili limeripoti kuhusu ziara ya Uhuru eneo la Ukambani Juni 28 na 29 mwaka huu. Hii ni baada ya kiongozi wa taifa kukutana na wajumbe kutoka kaunti za Kitui, Machakos na Makueni kuzungumzia maendeleo eneo hilo.

Viongozi hao walishikilia kuwa eneo la Ukambani linaunga mkono Ajenda Kuu Nne za maendeleo.

Uhuru atatembelea eneo hilo kati ya Juni 28 na Juni 29.

image

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.